Ijumaa, 29 Desemba 2023
Alhamisi, 28 Desemba 2023
Sabato Maana Yake ni Nini ? MAANA YA SABATO KIBIBLIA Ielewe Sabato ya Kweli
#FaidayaJaribu: #Usiogope
Ni Sehemu ya Kitabu Chetu Tarajiwa cha MAANA YA UZIMA, NA UZIMA WA MILELE.
Na Mwalimu Oscar samba
Pwenti ya Pumziko Kuu.
Kwenye Kipengele cha Taswira ya Uzima wa Milele
Pumziko Kuu; Yaani Sabato Kukuu. Watu wengi hawajui ya kuwa Sabato maana yake ni pumziko katika kilele cha uzima wa milele yaani wakati huu hapa ulimwenguni kwa kuokoka, (kupumzika katika Kristo Yesu kama mtua mizigo ya dhambi na kila mateso.) Na pili kama sehemu ya kupumzika kutoka katika dunia iliyopo chini ya umiliki wa Shetani kama mungu wa dunia hii, na pamoja na dunia yenye pigo la laana la kosa la Adamu na Hawa.
Unapookoka ni umeingia katika Sabato. Kwa hiyo, msabato halisi ni mtu aliyeokoka. Kama hujaokoka wewe sio Msabato, maana bado upo chini ya utumwa wa Shetani. Wokovu unakupa pumziko. Kanuni na sheria zile za Agano la Kale hususani sabato na taratibu zake zote, zilinuia kutufikisha hapa kwenye wokovu na hatimaye katika Sabato kamilifu ile ya Mbingu Mpya na Nchi Mpya.
Jumatano, 13 Desemba 2023
Ni Sehemu ya Kitabu Chetu Tarajiwa cha FIKRA SAHIHI KATIKA SHAMBA LA BWANA. Pwenti ya 18. 18. Ni Kiongozi Mwenye Mfumo wa Maisha, na Mfumo wa Uongozi Kama Mtumishi au Mtumikiaji na Sio Mtumikiwa. "Servanthood."
Mwalimu Oscar:
Mwl OSCAR SAMBA ( #NasahazaMwlOscar )
#FaidayaJaribu: #Usiogope
Ni Sehemu ya Kitabu Chetu Tarajiwa cha FIKRA SAHIHI KATIKA SHAMBA LA BWANA. Pwenti ya 18.
18. Ni Kiongozi Mwenye Mfumo wa Maisha, na Mfumo wa Uongozi Kama Mtumishi au Mtumikiaji na Sio Mtumikiwa. "Servanthood."
Huyu ni kiongozi ambaye sio bunyenye, kama aliyekuwa mkuu wangu wa chuo Mzee Marehemu Jonas Mkoba alivyopenda kusisitiza.
Huyu ni kiongozi ambaye hatafuti ukuu katika ulimwengu huu wala katika maisha yake ya kiuongozi. Anaishi maisha ya kujinyenyekeza au kujinyenyekesha kama mtoto. Yesu alilijua hili, na alilichukia na kulionya sana. Maana kanuni moja wapo yakuwa mkubwa mbinguni ni kuwa mdogo duniani. Aliwaambia wanafunzi wake ambao waliuliza swali zuri sana tu, ya kuwa ni nani aliye mkubwa mbinguni _ya kwamba huyo aliyemkubwa huko ni yule aliye mdogo huku au humu ulimwenguni.
Anaposema usipoongoka, uwe na hakika ananena habari za usipobadilika. Kuongoka ni kubadilika kwa nia ya kubadilisha fikra au akili zako ama mtazamo; ni katika mfumo au maana ya kutubu. Biblia moja wapo ya kiswahili yenye kutumia kiswahili kile chepesi imetumia maneno kubadilika au kubadilishwa. Linalolandana na Biblia kadhaa za kingereza.